Posts

Showing posts from December, 2015

HII NDIO TOP TEN YA MASHAIRI YA NYIMBO ZILIZOTAFUTWA SANA MTANDAONI MWAKA 2015

Image

MSIMAMO WA LIGI KUU BAADA YA MECHI ZA JANA NA JUZI

Image

MECHI ZA LEO LIGI KUU ENGLAND

Image

new audio vocalist beautiful

Image

Listen and Download ew music kutoka kwa Vocalist-ii love you

Image

Habari zilopo magazetini leo DEC 24

Image

Serikali yasitisha bomoabomoa kwa siku 14 kuwapa mda wa kuhama watu

Image
Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la  Msimbazi Mkwajuni kuondoka ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka  wenyewe. Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo  kinyume na sheria kwani kwa sabu ni mahali hatarishi.   Akaongeza kuwa kwanzi mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuvisimamia kwa ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.    katika eneo la Mkwajuni  makundi ya watu yanajitahidi kuhamaisha vitu vyao ili kuepusha uwezekano wa kupata hasara pindi tinga tinga litakapokuja huku wengine wakisema kuwa kuisha kwa muda ili kutoa nafasi watu kuhama ni jambo jema.   Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za bomoabomoa na kusema kuwa i

Tiger Woods kurejea uwanjani

Image
Mwanamichezo nguli aliyewahi kuwa mcheza golf namba moja duniani Tiger Woods, amesema kwamba ana matarajio ya kushinda michuano mikubwa zaidi katika kipindi cha miaka kumi ijayo. Woods, ambaye mwishoni mwa mwezi huu atatimiza umri wa miaka 40, amedondokea katika nafasi ya 414 katika viwango vya ubora wa mchezo wa golf duniani na alishinda taji lake la 14 kwa mara ya mwisho mnamo mwaka 2008. Tiger aliwahi kufanyiwa upasuaji wa mgongo mwezi September mwaka huu hiyo ikiwa ni mara ya pili katika kipindi cha miezi 18 lakini ana matarajio ya kucheza kwa ufanisi zaidi mwanzoni mwa mwaka mpya wa 2016. "Najiona wapi binafsi katika kipindi cha miaka mitano ama kumi ijayo? Alinukuliwa Tiger akisema na kuongeza kwamba bado ninao uwezo wa kucheza golf katika kiwango cha ubora wa hali ya juu na kushinda katika michuano mikubwa na kutwaa tuzo" na haya aliyaandika katika tovuti yake binafsi pia. Woods amejiwekea rekodi ya kushinda katika mchezo wa golfu kwa wiki mia sita theman

Mapinduzi cup kuanza Januari 2

Image
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar Kassim Haji Salum amesema Klabu za Gor Mahia ya kenya , KCCA ya Uganda , Yanga, Simba, Azam FC na Mtibwa sugar kutoka Tanzania Bara na Mafunzo na JKU kutoka visiwani Zanzibar ndio Timu zitakazoshiriki Mashindano ya Mapinduzi Cup Mashindano ambayo yanatarajiwa kuanza Januari 2 visiwani Humo.  Michuano ya Mapinduzi Cup itazisaidia Timu za Yanga, Azam FC, JKU na Mafunzo kujiandaa na Mashindano ya CAF ya Klabu Barani Afrika. Yanga watacheza michuano ya CAF Champion Ligi kwa kucheza mchezo wa mtoano na Timu ya Cercle de Joachim ya Mauritius wakati Azam FC watacheza na Mshindi kati ya Klabu ya Seychelles na Bidvest Wits ya Afrika Kusini katika Kombe la Shirikisho. Mafunzo ya zanzibar wao watacheza na klabu ya AS Vita ya Congo DR kwenye CAF Champion Ligi na Timu ya JKU itashiriki Kombe la Shirikisho pamoja na Gaborone United ya Botswana

Wachezaji 10 wanaoongoza kwa kutoa pasi za magoli Ligi Kuu Uingereza msimu huu

Image
hii ndio list inayongoza mpaka sasa

WATCH AND DOWNLOAD NEW VIDEO KUTOKA KWA OMMY DIMPOZ-ACHIA BODY

Image
DOWNLOAD HAPA ! AA!!!!!

WATCH AND DOWNLOAD NEW VIDEO KUTOKA KWA ALIKIBA x CHRISTIAN BELLA-NAGHARAMIA

Image
DOWNLOAD HAPAAAAAA!!!!!!!!

SUAREZ AIPELEKA BARCA FAINALI KATIKA KOMBE LA DUNIA LA VILABU

Image
Mshambuliaji Luis Suarez ameipeleka timu yake ya Barcelona, katika hatua ya fainali ya kombe la dunia la vilabu. Barcelona waliokua wakicheza dhidi ya Guangzhou Evergrande, walipata ushindi wa mabao 3-0 huku mshambuliaji nyota wa timu hiyo Luis Suarez akifunga mabao yote matatu. Suarez alianza kuandika bao la kwanza katika dakika ya 39 kisha akaongeza la pili dakika ya 50 na kuhitisha kazi kwa bao la tatu kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 67. Barcelona watachuana na River Plate katika mchezo wa fainali itayofanyika desemba 20 katika uwanja wa Yokohama nchini japan

Mourhino afutwa kazi chelsea rasmi

Image
Meneja wa klabu ya Chelsea ya Uingereza amefutwa kazi baada ya klabu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya. The Blues walishinda Ligi ya Premia msimu uliopita lakini msimu huu mambo yamekuwa kinyume, na wamo alama moja tu juu ya eneo la kushushwa daraja ligini. Bodi ya klabu hiyo ilikutana jana kujadili hatima ya Mourinho chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich. Klabu hiyo kupitia taarifa imesema mkataba kati ya klabu na meneja hiyo umekatishwa kwa maelewano kati ya pande zote mbili na ikamtakia kila la kheri Mourinho. “Sifa zake Stamfrod Bridge na Uingereza zinajieleza na daima anakaribishwa kurejea Stamford Bridge,” klabu hiyo imesema kupitia taarifa. “Sasa tutaangazia kuhakikisha kikosi chetu kilichojaa wachezaji wenye vipaji kinafikia uwezo wake. Hakutakuwa na taarifa zozote zaidi kutoka kwa klabu hadi kocha mpya ateuliwe.” Bodi ya Chelsea yamjadili Mourinho Guardiola kuweka wazi hatima Mourinho: Naona aibu Mreno huyo mwenye umri wa mi

Utafiti: Watanzania wana wasiwasi kuhusu mashambulizi

Image
Matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Twaweza yanaonyesha zaidi ya 80% ya Watanzania wanaona nchi yao iko salama kutoka kwa vitendo vya makundi yenye itikadi kali. Utafiti huo wa maoni ulifanywa kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu ukitaka kujua mtazamo wa wananchi juu ya hali ya vitendo vya itikadi kali nchini. Kwa mujibu wa utafiti huo, ingawa wananchi wengi wanajihisi kuwa salama, takribani asilimia 56 wana wasiwasi juu ya vitisho vya mashambuliz dhidi ya Tanzania katika siku zijazo. Hata hivyo Meja Jenerali Venansi Mabeo, ambaye ni mkuu wa usalama katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania ameondoa wasiwasi huo na kusema hali ya usalama si ya kutia shaka. Wakizungumzia sababu zinazowashawishi watu wengi kuvutiwa na itikadi hizi, wananchi wengi wamesema ukosefu wa ajira, utawala mbovu pamoja na kukatishwa tamaa na mifumo ya serikali ni mambo yanayoongoza katika ushawishi huo Kwa upande mwingine, wananchi katika ripoti hiyo wamesema wanapend

WANYARWANDA WASHIRIKI KURA YA MAONI LEO

Image
Raia wa Rwanda wameanza kufika vituoni kushiriki kwenye kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi na mapema, huku watu 6 milioni wakitarajiwa kupiga kura. Bw Kagame anatarajiwa kupiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali. Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.  Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017. Lakini kiongozi huyo ameyashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.  Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa. Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa rais kuto

WATCH AND DOWNLOAD Izzo Bizness ft Mwana FA G Nako Shem Lake Official Music Video

Image
                                                                DOWNLOAD HAPAAAA

WAZIRI WA KILIMO NA UFUGAJI MH.MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAKULIMA WA KOROSHO KULIPWA NDANI YA SAA 48

Image
Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mh.Mwigulu Lameck Nchemba atoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway ltd kulipa Billion 3.4 kwa wakulima wa korosho Mkoa wa pwani. Kufuatia agizo hio,Wakulima waliouza korosho hiyo wataanza kulipwa jumatatu ya tar.21.12.2015

TP Mazembe WASHINDWA TENA JAPAN

Image
Mabingwa wa soka Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamecharazwa 2-1 na Club America ya Mexico katika michuano ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu.  Mechi hiyo ilikuwa ya kuamua nani angemaliza nambari tano katika fainali hizo ambazo zinachezewa Japan. Dario Benedetto na Martin Zuniga walifunga mabao mawili kipindi cha kwanza na kuwaweka mabingwa hao wa Concacaf kwenye udhibiti wa mechi hiyo. Rainford Kalaba alikombolea mabingwa wa Afrika mechi moja zikiwa zimesalia dakika mbili kabla ya mechi kuisha. TP Mazembe yachapwa 3-0 Klabu Bingwa Duniani Samatta katika orodha ya 3 bora ya CAF Samatta, kijana anayevumisha soka ya Tanzania Lakini mabingwa hao hawakuweza kujikwamua na safari yao kwenye michuano hayo iliisha kwa masikitiko. Kabla ya mechi hiyo, Mazembe walikuwa wamechapwa 3-0 na Sanfrecce Hiroshima kutoka Japan hatua ya robofainali, kwenye mechi iliyochezewa mjini Osaka Jumapili.

UEFA YATAJA WAAMUZI 18 Euro 2016

Image
Kamati ya Marefa ya shirikisho la soka barani ulaya Uefa imeteua waamuzi 18 kwa ajili ya michuano ya ulaya itakayofanyika huko nchi Ufaransa mwaka 2016. Waamuzi hao watachezesha michezo 51 ya michuano hiyo ya ulaya itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 10 na kumalizika Julai 10 mwaka 2016. Katika kila mchezo mmoja watatumika waamuzi watano kama iliyokua katika michuano ya Euro ya mwaka 2012, kutakua na mwamuzi wa kati akisaidiwa na waamuzi wawili wa pembeni na wengine wawili katika kila goli. Orodha ya mwisho ya waamuzi watakaochezesha fainali hizo itatolewa mwezi Februari mwakani na kamati hiyo ya waamuzi.

MESSI NEYMAR NJE KIKOSI BORA UEFA

Image
Kikosi bora cha wachezaji kumi na mmoja kilichocheza hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kimetangazwa na Uefa jambo la kushangaza likiwa kuachwa nje kwa nyota wa Barcelona Lionnel Messi, Neymar na Luis Suarez. Washambuliaji Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Hulk (Zenit St Petersburg) pamoja na Thomas Muller (Bayern Munich) ndio wanaoongoza safu ya ushambuliaji, kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3. Ligi Kuu ya Uingereza imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa. Mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona, hawajatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji. Kikosi kamili ni: Kipa: Kevin Trapp (Paris Saint-Germain Mabeki: Andrea Barzagli (Juventus),Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Diego Godin (Atletico Madrid), David Alaba (Bayern Munich) Viungo wa Kati: Sven Kums (Gent), Willian (Chelsea), Raheem Sterling (Manchester City) Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Muni

Trump akosolewa mdahalo wa Republican

Image
Wagombea wa Republican waWagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia. Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani. Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, amemwita “mgombea wa vurugu”. Seneta Marco Rubio na Ted Cruz pia wametofautiana kuhusu juhudi za serikali kupeleleza raia wake. “Hatuzungumzi kuhusu kutengwa kwa watu, tunazungumzia usalama,” amejitetea Bw Trump. “Hatuzungumzi kuhusu dini, tunazungumza kuhusu usalama.” Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu Mjadala huo upesi ulipanuka na kuan

Thiery Henry ndiye mchambuzi wa soka kwenye TV anayelipwa fedha nyingi zaidi UK

Image
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa, Thiery Henry ndiye mchambuzi wa soka anayelipwa fedha nyingi zaidi nchini Uingereza. Sky Sport wanamlipa pauni milioni nne kila mwaka katika mkataba wake wa miaka sita. Pamoja na kuwa nao, mkataba wake unamruhusu kufanya kazi hiyo na vituo vya runinga vingine.Tayari imefahamika kuwa BBC Sport wanatarajia kumtangaza kama mchambuzi wao wa European Championship.

Lipstick za Drake zamalizika dakika moja tu baada ya kuingia sokoni

Image
Lipstick za Drake kupitia brand ya Tom Ford zimemalizika dakika moja tu baada ya kuingia sokoni. Lipstick hizo ni sehemu ya collection ya Tom Ford, Lips & Boys. Kupitia Instagram, Drake amepost picha hiyo juu na kuandika:" My mom bought all of them. Hey Ma.” Lipstick hizi zilikuwa zikiuzwa kwa $35.

MELI YA MV ROYAL YAWAKA MOTO BAHARI YA HINDI

Image
MOTO  UKIZIMWA Meli ya MV Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba imewaka moto leo ikiwa majini katika Bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba chanzo cha moto huo ni hitilafu iliyotokea katika injini ya meli hiyo. Meli ya MV Serengeti iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja inaendelea na zoezi la uokoaji katika meli hiyo.  Baadhi ya abilia wakitolewa kutoka kwenye meli ya MV ROYAL kwenda MV SERENGETI

Mapya yaibuka kashfa mabilioni ya uingereza

 Kashfa ya ufisadi kwenye mauzo ya hati fungani za Dola 600 (sawa na Sh. trilioni 1.3) ambazo Serikali ya Tanzania iliziuza kwa Benki ya Standard ya Uingereza mwaka 2012 imeingia sura mpya baada ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Kupambana na Rushwa ya Uingereza (Corruption Watch), kutaka wahusika wa sakata hilo washitakiwe mahakamani. Kwa mujibu wa taarifa ya Corruption Watch iliyotolewa na Nipashe kupata nakala yake jana, ilipinga kitendo cha watuhumiwa wa suala hilo kuachwa kufuatia uamuzi wa makubaliano ya mahakamani (DPA) kati ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa Kubwa ya Uingereza (SFO) na Benki ya Standard Novemba 30, mwaka huu. Mahakama ya Crown Court Southwark ya jijini London, Uingereza, Novemba 30, mwaka huu iliamuru Serikali ya Tanzania irejeshewe Dola za Marekani milioni sita (sawa na Sh. bilioni 12.6) kutokana na kubainika kuwapo kwa udanganyifu baada ya kesi hiyo kufunguliwa kwenye mahakama ya kwamba asilimia moja ya mkopo huo ambayo ni Dola milioni sita zililipwa kwa

MBARONI KWA KUMFUNGIA NDANI MTOTO KWA MIAKA 12

Image
POLISI mkoani Singida inamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Itaja na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani ya chumba mtoto wao mlemavu wa viungo kwa miaka 12 bila kutoka nje. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni David Mtipa (59) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa hilo na mkewe Mariam Philipo (45) wote wakazi wa kijiji cha Itaja katika tarafa ya Mgori wilayani Singida. Kamanda Sedoyeka alisema tukio hilo liligundulika juzi katika kijiji hicho baada ya Polisi kupata taarifa za siri kutoka kwa wasamaria.     Akielezea tukio hilo, Kamanda Sedoyeka alisema watuhumiwa walimfungia ndani ya chumba mtoto huyo, Timotheo David (30) kwa muda wa miaka 12 huku huduma zote za kibinadamu, ikiwemo haja ndogo na kubwa pamoja na chakula zikifanyika humo ndani. “Baada ya timu ya askari wa Upelelezi na Ofisa Ustawi wa Jamii kufika eneo hilo wakiwa na viongozi wa kijiji na kufanya mahojiano, watuhumiwa walikiri kumfungia chumbani mtoto wao

LOWASA KUZUNGUKA TANZANIA NZIMA KUWASHUKURU WA TATANZANIA KWA KUMPIGIA KURA

Image
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga. Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani. Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. “Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa