Posts

Showing posts with the label NEWS

Matokeo ya kidato cha pili mwaka 2015/2016

Image
    <<<<<<CLICK HERE KUYAONA>>>>

SUMATRA WAWATAKA WANANCHI WAKATOE MAONI YAO KUHUSU NAULI PENDEKEZWA KWA MABASI YAENDAYO KASI

Image

Serikali yasitisha bomoabomoa kwa siku 14 kuwapa mda wa kuhama watu

Image
Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la  Msimbazi Mkwajuni kuondoka ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka  wenyewe. Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo  kinyume na sheria kwani kwa sabu ni mahali hatarishi.   Akaongeza kuwa kwanzi mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuvisimamia kwa ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.    katika eneo la Mkwajuni  makundi ya watu yanajitahidi kuhamaisha vitu vyao ili kuepusha uwezekano wa kupata hasara pindi tinga tinga litakapokuja huku wengine wakisema kuwa kuisha kwa muda ili kutoa nafasi watu kuhama ni jambo jema.   Aidha baadhi ya wananchi wameponge...

Utafiti: Watanzania wana wasiwasi kuhusu mashambulizi

Image
Matokeo ya utafiti uliofanywa na shirika la kijamii la Twaweza yanaonyesha zaidi ya 80% ya Watanzania wanaona nchi yao iko salama kutoka kwa vitendo vya makundi yenye itikadi kali. Utafiti huo wa maoni ulifanywa kati ya mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu ukitaka kujua mtazamo wa wananchi juu ya hali ya vitendo vya itikadi kali nchini. Kwa mujibu wa utafiti huo, ingawa wananchi wengi wanajihisi kuwa salama, takribani asilimia 56 wana wasiwasi juu ya vitisho vya mashambuliz dhidi ya Tanzania katika siku zijazo. Hata hivyo Meja Jenerali Venansi Mabeo, ambaye ni mkuu wa usalama katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi la Tanzania ameondoa wasiwasi huo na kusema hali ya usalama si ya kutia shaka. Wakizungumzia sababu zinazowashawishi watu wengi kuvutiwa na itikadi hizi, wananchi wengi wamesema ukosefu wa ajira, utawala mbovu pamoja na kukatishwa tamaa na mifumo ya serikali ni mambo yanayoongoza katika ushawishi huo Kwa upande mwingine, wananchi katika ripoti hiyo wamesema wanapend...

WANYARWANDA WASHIRIKI KURA YA MAONI LEO

Image
Raia wa Rwanda wameanza kufika vituoni kushiriki kwenye kura ya maoni ya marekebisho ya katiba, ambayo yakiidhinishwa yatamruhusu Rais Paul Kagame kuwania urais kwa muhula wa tatu. Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa asubuhi na mapema, huku watu 6 milioni wakitarajiwa kupiga kura. Bw Kagame anatarajiwa kupiga kura katika kituo cha Rugunga mjini Kigali. Mabadiliko hayo yakiidhinishwa, huenda yakamuwezesha Bw Kagame kusalia madarakani hadi 2034.  Marekani imetoa wito kwa Bw Kagame kuonyesha uzalendo na kuondoka madarakani muda wake ukimalizika mwaka 2017. Lakini kiongozi huyo ameyashambulia mataifa yanayotoa wito huo, akisema yanaingilia maswala ya ndani ya taifa hilo la Afrika Mashariki. Mwezi uliopita, Bunge la Seneti nchini Rwanda liliidhinisha marekebisho hayo na kupisha kuandaliwa kwa kura ya maoni.  Bw Kagame atakuwa radhi kuwania urais kwa muhula mwingine wa miaka 2017 marekebisho yakiidhinishwa. Hata ingawa marekebisho hayo yanapunguza muda wa muhula wa ...

WAZIRI WA KILIMO NA UFUGAJI MH.MWIGULU NCHEMBA AAGIZA WAKULIMA WA KOROSHO KULIPWA NDANI YA SAA 48

Image
Waziri wa Kilimo Uvuvi na Mifugo Mh.Mwigulu Lameck Nchemba atoa saa 48 kwa kampuni ya Sparkway ltd kulipa Billion 3.4 kwa wakulima wa korosho Mkoa wa pwani. Kufuatia agizo hio,Wakulima waliouza korosho hiyo wataanza kulipwa jumatatu ya tar.21.12.2015

Trump akosolewa mdahalo wa Republican

Image
Wagombea wa Republican waWagombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani wamejibizana kuhusu njia bora zaidi za kudumisha usalama wa taifa na kukabiliana na Islamic State (IS) kwenye mdahalo wa kwanza tangu kutokea kwa mashambulio ya California na Paris. Mgawanyiko mkubwa umetokea kati ya wale wanaotetea kuwepo kwa upeelezi zaidi na wale wanaotetea haki za kiraia. Mgombea anayeongoza, Donald Trump, amelazimika kujitetea kutokana na pendekezo lake kwamba Waislamu wazuiwe kuingia Marekani. Mgombea mmoja anayempinga vikali, Jeb Bush, amemwita “mgombea wa vurugu”. Seneta Marco Rubio na Ted Cruz pia wametofautiana kuhusu juhudi za serikali kupeleleza raia wake. “Hatuzungumzi kuhusu kutengwa kwa watu, tunazungumzia usalama,” amejitetea Bw Trump. “Hatuzungumzi kuhusu dini, tunazungumza kuhusu usalama.” Trump: Dunia ingekuwa bora na Gaddafi na Saddam Mambo 20 makuu anayoamini Donald Trump Trump akemewa kwa matamshi kuhusu Waislamu Mjadala huo upesi ulipanuka na kuan...

Lipstick za Drake zamalizika dakika moja tu baada ya kuingia sokoni

Image
Lipstick za Drake kupitia brand ya Tom Ford zimemalizika dakika moja tu baada ya kuingia sokoni. Lipstick hizo ni sehemu ya collection ya Tom Ford, Lips & Boys. Kupitia Instagram, Drake amepost picha hiyo juu na kuandika:" My mom bought all of them. Hey Ma.” Lipstick hizi zilikuwa zikiuzwa kwa $35.

MELI YA MV ROYAL YAWAKA MOTO BAHARI YA HINDI

Image
MOTO  UKIZIMWA Meli ya MV Royal iliyokuwa ikitokea Unguja kuelekea Pemba imewaka moto leo ikiwa majini katika Bahari ya Hindi. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ni kwamba chanzo cha moto huo ni hitilafu iliyotokea katika injini ya meli hiyo. Meli ya MV Serengeti iliyokuwa ikitokea Pemba kuelekea Unguja inaendelea na zoezi la uokoaji katika meli hiyo.  Baadhi ya abilia wakitolewa kutoka kwenye meli ya MV ROYAL kwenda MV SERENGETI

Mapya yaibuka kashfa mabilioni ya uingereza

 Kashfa ya ufisadi kwenye mauzo ya hati fungani za Dola 600 (sawa na Sh. trilioni 1.3) ambazo Serikali ya Tanzania iliziuza kwa Benki ya Standard ya Uingereza mwaka 2012 imeingia sura mpya baada ya taasisi isiyo ya kiserikali ya Kupambana na Rushwa ya Uingereza (Corruption Watch), kutaka wahusika wa sakata hilo washitakiwe mahakamani. Kwa mujibu wa taarifa ya Corruption Watch iliyotolewa na Nipashe kupata nakala yake jana, ilipinga kitendo cha watuhumiwa wa suala hilo kuachwa kufuatia uamuzi wa makubaliano ya mahakamani (DPA) kati ya Taasisi ya Kupambana na Rushwa Kubwa ya Uingereza (SFO) na Benki ya Standard Novemba 30, mwaka huu. Mahakama ya Crown Court Southwark ya jijini London, Uingereza, Novemba 30, mwaka huu iliamuru Serikali ya Tanzania irejeshewe Dola za Marekani milioni sita (sawa na Sh. bilioni 12.6) kutokana na kubainika kuwapo kwa udanganyifu baada ya kesi hiyo kufunguliwa kwenye mahakama ya kwamba asilimia moja ya mkopo huo ambayo ni Dola milioni sita zililipwa ...

MBARONI KWA KUMFUNGIA NDANI MTOTO KWA MIAKA 12

Image
POLISI mkoani Singida inamshikilia Mchungaji wa Kanisa la Pentekoste Itaja na mkewe kwa tuhuma za kumfungia ndani ya chumba mtoto wao mlemavu wa viungo kwa miaka 12 bila kutoka nje. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni David Mtipa (59) ambaye ni Mchungaji wa Kanisa hilo na mkewe Mariam Philipo (45) wote wakazi wa kijiji cha Itaja katika tarafa ya Mgori wilayani Singida. Kamanda Sedoyeka alisema tukio hilo liligundulika juzi katika kijiji hicho baada ya Polisi kupata taarifa za siri kutoka kwa wasamaria.     Akielezea tukio hilo, Kamanda Sedoyeka alisema watuhumiwa walimfungia ndani ya chumba mtoto huyo, Timotheo David (30) kwa muda wa miaka 12 huku huduma zote za kibinadamu, ikiwemo haja ndogo na kubwa pamoja na chakula zikifanyika humo ndani. “Baada ya timu ya askari wa Upelelezi na Ofisa Ustawi wa Jamii kufika eneo hilo wakiwa na viongozi wa kijiji na kufanya mahojiano, watuhumiwa walikiri kumfungia chumb...

LOWASA KUZUNGUKA TANZANIA NZIMA KUWASHUKURU WA TATANZANIA KWA KUMPIGIA KURA

Image
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa ataanza ziara ya kuzunguka nchi nzima kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na kesho atakuwa Tanga. Katika ziara hiyo, Lowassa ataambatana na viongozi waandamizi wa Chadema na Ukawa kuwashukuru wananchi kwa namna walivyounga mkono upinzani na ajenda nzima ya mabadiliko katika Uchaguzi Mkuu uliopita. Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema, Tumaini Makene imesema kiongozi huyo atatoa shukrani zake kwa wananchi kwa jinsi wanavyoendelea kuweka matumaini yao kwa upinzani. Taarifa hiyo ilieleza kwamba wananchi bado wanaamini kwamba upinzani ndiyo nguzo imara wanayoitegemea katika kuwaletea mabadiliko ya kweli kwa ajili ya maendeleo yao na ustawi wa Taifa kwa ujumla. “Wananchi wanastahili shukrani kwa imani hiyo kubwa ambayo ni ishara ya wazi kuwa matumaini yao kwa ...

SOMA KILICHOANDIKWA MAGAZETINI LEO TAREHE 11/12/2015

Image
SOMA HAPAAAAAA!!!!!!!!!!!!!

HILI NDILO BARAZA JIPYA LA MAAZIRI

Image
Jumla ya wizara ni 18 , Mawaziri ni 19. Wizara ya Mambo ya Nje na EAC/ Kimataifa - Augustino Mahiga, Naibu Waziri - Dk. Suzan Kolimba Wazara wa Utamaduni, Sanaa na michezoWaziri-Nape Nnauye Wizara ya Nishati na Madini Waziri -Sospeter Muhongo na Naibu Waziri-Medard Kalemani Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Waziri -Jenista Mhagama Wizara ya ofisi ya Rais, Utumishi na utawala mawaziri wawili - Simbachawene na Kairuki Ofisi ya Makamu wa Rais/Muungano na Mazingira Waziri - January Makamba Naibu waziri Luhaga Mpina . Wizara ya Mambo ya Ndani Waziri ni Charles Kitwanga Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi Waziri wake ni Wiliam Lukuvi Naibu Angelina Mabula . Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Waziri - Husein Mwinyi Wizara ya Katiba na Sheria Waziri - Harrison Mwakyembe Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Waziri - January Makamba Wizara ya kilimo, mifugo na uvuvi Waziri- Mwigulu Nchem...

SOMA YALIOJIRI KWENYE MAGEZETI LEO

Image
SOMA HAPAA!!!!!!!