Serikali yasitisha bomoabomoa kwa siku 14 kuwapa mda wa kuhama watu

Serikali imesitisha zoezi la bomoabomoa kwa muda wa siku 14 ili kuwapa muda wa kutosha watu waliovamia na kuishi katika bonde la  Msimbazi Mkwajuni kuondoka ambapo imesisitiza kuwa baada ya siku hizo kuisha zoezi hilo litaanza tena na hivyo wahakikishe wanaondoka  wenyewe.
Akitoa tamko hilo waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh William Lukuvi amesema waliojenga katika eneo hilo wapo hapo  kinyume na sheria kwani kwa sabu ni mahali hatarishi.
 
Akaongeza kuwa kwanzi mwakani wizara yake itagawa kwa viongozi wa serikali za mitaa ramani za mipango miji ili waweze kuvisimamia kwa ukaribu ili kuepusha uwezekano wa kutokea ama kufanya ujezi holela.
 
 katika eneo la Mkwajuni  makundi ya watu yanajitahidi kuhamaisha vitu vyao ili kuepusha uwezekano wa kupata hasara pindi tinga tinga litakapokuja huku wengine wakisema kuwa kuisha kwa muda ili kutoa nafasi watu kuhama ni jambo jema.
 
Aidha baadhi ya wananchi wamepongeza zoezi za bomoabomoa na kusema kuwa imekuwa na hatua ngumu lakini muhimu kwani eneo hilo limekuwa likisababisha vifo vya watu kila mafuriko yanapotokea hivyo watu kuondolewa hapo wamenusurishwa kwa mengi.
 
Katika hatua nyingine waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Mh Jenister Mhagama ameziagiza kamati za maafa katika ngazi za mikoa, wilaya na vijiji kuorodhesha na kuwapa barua za kuwataka watu wote wanaoishi maeneo hatarishi kuhama mara moja katika maeneo hayo na utekelezaji wa agizo hilo uwasilishwe ofisi ya waziri mkuu haraka iwezekanavyo

Comments