TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA
Dirisha la usajili wa majira ya baridi Ulaya la Januari linakaribia kufunguliwa timu nyingi zinajipanga kifedha kuhakikisha zinakuwa na nguvu ya kuingia sokoni.
Arsenal ipo kwenye mazungumzo na nyota wa Kibrazili
Arsenal wanajipanga kuanza mazungumzo na Palmeiras kuhusu uhamisho wa nyota Mbrazili mwenye umri wa miaka 18, mshambuliaji Gabriel Jesus.
Chelsea & Spurs zamwania Berahino
Chelsea na Tottenham zinamfuatilia kwa karibu sana Saido Berahino, zimekuwa zikichunguza mwenendo wake baada ya mshambuliaji huyo kucheza dakika zote katika kikosi cha West Brom umri chini ya miaka 21.
Juve inajipanga kumsajili 'Pogba mpya'
Juventus imekubali kufanya dili la kumsajili kiungo wa Modena, Emmanuel Besea. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 ambaye anayetajwa kuwa Paul Pogba mpya atajiunga na klabu ya Juve kwa mkopo kwanza lakini ikipewa fursa ya kumsajili moja kwa moja.
Palace inaisaka saini ya Batshuayi
Crystal Palace inaandaa kitita cha paundi milioni 15 kumsajili straika wa Marseille Mitchy Batshuayi.
Arsenal yamfuatila Insigne
Arsenal wanakaza macho kumfuatilia Lorenzo Insigne, Arsene Wenger anatamani sana kumsajli straika huyo wa Napoli.
Klopp anamtani Rossi
Jurgen Klopp amemtaja straika wa Fiorentina, Giuseppe Rossi kuwa moja ya wachezaji anaotaka kuwasajili dirisha la uhamisho wa Januari. Liverpool wanajipanga kumtengea kitita cha euro milioni 25 kumsajili nyota huyo wa zamani wa Manchester United.
Manchester United yatenga kitita cha paundi milioni 143.9 kumsajili Neymar
Imeripotiwa kuwa Manchester United imeshatenga kitita cha paundi mlioni 143.9 kwa ajili ya nyota wa Barcelona Neymar, ambaye inasadikika klabu hiyo inatafuta namna ya kumuuza kutokana na madai makubwa ya ujira.
Liverpool inamsaka Hummels
Habari zinadai kuwa The Reds wapo tayari kutoa ofa nono kuipata saini ya beki mahiri wa kati wa Borussia Dortmund, Mats Hummels.
Comments
Post a Comment